25 Agosti 2012 - 19:30

Kikao cha wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na upande Wowote wa Siasa NAM kimeanza leoTehran, Wanachama hao kutoka zaidi ya nchi 120 za kimataifa watashiriki katika kikao hicho.

Ali Akbar Salehi Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran akihutubia katika ufunguzi wa kikao hicho na kusisitiza juu ya nafasi muhimu iliyokua nayo Jumuiya ya NAM katika kutatua migogoro ya kisiasa na kiuchumi na kuzikurubisha pamoja nchi wanachama. Kikao cha  Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na upande Wowote   wa Siasa NAM kinamalizika kesho na kupisha kikao cha Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa jumuiya hiyo kabla ya kilele cha mkutano huo cha wakuu wa jumuiya hiyo kitakachofanyika katika siku ya Akhamisi na Ijumaa.